Siri ya kufanikisha biashara yako

Image caption Maybin alianza kwa kuuza CD kabla ya kuwa wakala wa kuuza bima

Maybin Mudenda, alijikita kwenye biashara ya CD ili kujipatia pesa kwa ajili ya matumizi kabla ya kuwa wakala wa mauzo wa bima.

Katika sehemu ya mfululizo wa Makala za Ndoto ya Afrika, mfanya biashara huyu ambaye sasa anamiliki mradi wa kilimo cha Ngano mjini Chisamba na Insieme, mradi ambao unamiliki 50% ya hisa ya Kampuni ya African Grey na asilimia 20 ya hisa za Kampuni ya Genesis Finance.

Anatoa maelezo ya mafaniko ya mradi wake kwa wale wanaotaka kuimarisha biashara zao na kutoa mawazo kuhusu namna ambavyo Serikali inaweza kusaidia.

Hapa anaeleza namna ya kupata msaada wa kifedha ;

  • Fahamu wazo la kibiashara:mara kadhaa wajasiriamali wadogo hushindwa kujenga wazo, ili kupata soko kwa muwekezaji ni vyema kutangaza wazo la kipekee.
  • Usiharakishe:Wajasiriamali hufanya haraka kuwasilisha wazo la biashara.kwanza, wazo lazima lifanyiwa utafiti wa kina na kupanga kabla ya kuwasilisha kwa Mwekezaji.
  • Jiamini: Mwekezaji kutokuwa na imani na wajasiriamali wadogo , sababu inaweza kuwa sababu wajasiriamali hukosa kujiamini, hakuna anayekubali kuwekeza pesa kwa mtu asiye mwamini na asiyejiamini.Uoga ni kikwazo kikubwa cha mafanikio.
  • Jifunze kutokana na makosa: Njia muhimu ya kumtathimini mjasiriamali ni kutazama namna anavyo chukulia kuanguka kwake kibiashara, Wajasiriamali wengi hawajifunzi kutokana na makosa .
Image caption Anasema sehemu kubwa ya kuafinikisha biashara ni serikali kusaidia wajasiriamali

Namna Serikali inavyoweza kusaidia;

  • Kuondoa Urasimu:kukabiliana na urasimu wa Serikali ni tatizo kubwa kuliko yote kwa wafanyabiashara ndogo ndogo nchini Zambia na huenda na kwingineko barani Afrika, kurahisha taratibu za ulipaji kodi na usajili wa Kampuni kwa biashara ndogondogo kutaweza kuwasaidia wajasiriamali kukua haraka kibiashara na kuanza kuajiri wafanyakazi.

Wizara ya kushughulikia Biashara ndogo ndogo:Nchi nyingine za Afrika , ikiwemo Zambia , hazina budi kuiga mfano wa Afrika Kusini katika kuunda Wizara inayoshughulikia maendeleo ya biashara ndogondogo ili kuwasaidia wajasiriamali kuboresha bidhaa zao.

Kufugua milango:Serikali zinapaswa kusaidia wafanyabiashara kwa kuwashauri kuhusu faida za masoko mapya na kusaidia soko la bidhaa zao kupatikana.