Matatani kwa kumvua nguo mwanamke Kenya

Image caption Maandamano yalifanywa mjini Nairobi kupinga vitendo vya kuwavua nguo wanawake wanaovalia nguo fupi

Wafanyakazi wa basi moja waliotuhumiwa kwa kumnyanyasa kimapenzi mwanamke wanakabiliwa na hukumu ya kifo baada ya kushitakiwa kwa kosa la wizi wa mabavu.

Watu watatu wakiwemo wafanyakazi wanaofanya kazi katika basi hilo walikamatwa mwezi jana baada ya mwanamke huyo kujitoza na kusidia polisi kwuatambua watu waliomvamia.

Kanda ya video iliosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya na kusababisha maandamano ya wanawake nchini Kenya akiwasihi kutombaka na kuingiza chupa katika sehemu zake za siri.

Hata aliwasihi awape pesa wakati walipokuwa wanamtisha lakini wakakataa.

Mamia ya waandamanaji waliandamana mjini Nairobi baada ya tukio hilo na kulaani kitendo cha wanaume kuwavua wanawake nguo kwa kisingizio kuwa wamevalia nguo fupi sana au vimini hasa katika vituo vya basi.

Maandamano hayo yalipangwa kupitia kwa mtandao wa kijamii. Kauli mbiu ya maandamano hayo ilikuwa #MyDressMychoice yaani nitavalia kama nipendavyo.

Polisi walilazimika kubuni kikosi cha kuchunguza wale wanaowavua wanawake nguo zao kwa madai kuwa wamevalia nguo fupi sana.

Takriban wanawake watano wamevuliwa nguo zao mjini Nairobi na katika mji wa Mombasa pwani ya Kenya.

Polisi mmoja wa utawala alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kumvua nguo mwanamke mjini Nairobi.

Serikali ya Kenya imesema itafuta leseni za kampuni za basi ambazo wafanyakazi wake wanapatikana na hatia ya kuwavua nguo wanawake.