Soko la Nguo lashambuliwa Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa Boko Haram ambao wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Nigeria

Bomu limelipuka karibu na soko katika mji wa Kaskazini mjini mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa maafisa wakuu wanasema bomu hilo lilipuka katika eneo ambako mizigo hupakiwa, katika soko la nguo la Kantini Kwari.

Taarifa za majeruhi bado hazijatolewa. Takriban watu 2,000 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram mwaka huu.

Mwezi jana zaidi ya watu 100 walifariki katika shambulizi lengine lililofanywa na kundi hilo wakati wa maombi katika msikiti mkubwa mjini Kano.

Mwandishi wa BBC Habiba Adamu anasema Kantin Kwari ni soko kubwa zaidi la nguo mjini Kano ambako watu kutoka nchi jirani na maeneo mengine ya nchi kuendeshea biashara zao.

Soko hilo daima huwa limejaa watu.