Maandalizi ya kombe la Afrika yaendelea

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Uwanja wa Mpira na wachezaji

Zikiwa zimesalia takriban wiki tano kuanza rasmi kwa michuano ya kombe la Afrika,huko Equatorial Guinea ambao ni wenyeji wa mashindano hayo ,maandalizi yamepamba moto ambapo viwanja viwili tu ndo viko tayari kati ya vinne vitakavyotumika.

Morocco ilijitoa kama mwenyeji kwa hofu ya ugonjwa wa Ebola kufika nchini humo.

Viwanja vilivyokamilika ni katika mji mkuu Malabo na Bata ambao ni mji wa pili kwa ukubwa.

Lakini imekua ngumu kujenga viwanja vingine kuanzia mwanzo katika majimbo ya Mongomo na Ebebiyin, kaskazini mwa nchi.

Wakandarasi wamepewa sehemu mbalimbali kukamilisha kazi ya ujenzi kama vile vyoo ,bafu,milango pamoja na mapaa. Hata hivyo kazi hiyo inaonekana kuendelea polepole

Kumekua na wasiwasi kwa uwanja wa Mongomo wenye uwezo wa kuchukua watu 10,000,kama utakuwa tayari kwa muda wa kuanza kwa michuano ya kombe la Afrika.

Vigogo kumi na sita wa soka barani Afrika wakiongozwa na mwenyeji Equatorial Guinea watachuana kuwania ubigwa wa Afrika kuanzia January 17.