Waziri mpalestina auawa katika maandamano

Image caption Mwili wa waziri Ziad Abu Ein

Waziri wa mpalestina amefariki kufuatia mgogoro na wanajeshi wa Israel katika maandamano yaliyofanywa katika Ukingo wa Magharibi.

Madaktari wa kipalestina waliambia BBC kuwa Ziad Abu Ein, alifariki baada ya kurushiwa gesi ya kutoa machozi wakati wa makabiliano na asakri wa kiyahudi karibu na kijiji cha Turmusaya.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Picha zilimuonyesha Ziad Abu Ein akikabiliana na wanajeshi wa Israel

Lakini watu kadhaa walioshuhudia vurugu hizo walisema waziri huyo aligongwa na askari hao na hata kusukumwa.

Mmoja alidai kua aligongwa kifuani mwake nkwa mkebe wenye gesi ya kutoa machozi.

Jeshi la Isrsel linasema kuwa linachunguza madai hayo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Waandamanaji wa walitaka kupanda mti wa mzaituni katika sehemu moja ya ardhi wakihofia kuwa Israel itanyakua ardhi hio

Tukio la leo linakuja wakati hali ya taharuki ikitanda kati ya waisraeli na wapalestina.

Katika wiki za hivi karibuni wanajeshi 11 wameuawa na wapalestina wakiwemo watano waliodungwa kisu na wengine kupigwa risasi wakiwa katika sinagogu mjini Jerusalem.

Wapalestina13 pia waliuawa baadhi yao wakiwa washambuliaji.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Walipokaribia eneo hilo polisi wa Israel wakaanza kuwafukuza

Bwana Abu Ein,alikuwa waziri bila cheo maalum, na alikuwa miongoni mwa wanaharakati wapalestina walioshiriki maandamano Jumanne asubuhi kupinga unyakuzi wa ardhi ili kuzuia ujenzi wa makazi ya walowezi.

Wakati wa maandamano yao ndipo walipokabiliana na kikundi cha wanajeshi 15 wayahudi.

Mwandishi wa BBC mjini Jerusalem anasema kuwa huenda wapalestina wakaona mauaji hayo kama ishara au dalili ya kuzorotesha uhusiano zaidi katika eneo hilo.