Ebola bado tishio Sierra Leone

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shughuli za mazishi hufanywa kwa makini kuepuka maambukizi ya Ebola

Maafisa wa Afya nchini Sierra Leone wamegundua miili kadhaa katika maeneo ya mgodi wa Almasi, na kusababisha hofu kuwa pengine ugonjwa wa Ebola haujaripotiwa ipasavyo.

Shirika la afya duniani,WHO limesema limebaini kisa hiki kipya mashariki mwa mji wa Kono, timu ya Wataalamu imepelekwa Kono kufanya uchunguzi kuhusu uwepo wa ugonjwa wa Ebola.

Watu 6,346 wamepoteza maish akutokana na ugonjwa huo na zaidi ya 17,800 wameathirika na Ebola.

Sierra Leone ina idadi kubwa zaidi ya Watu wenye Ebola Afrika Magharibi, ikiwa na Watu walioathirika 7,897 tangu kuanza kwa ugonjwa huo.

WHO imesema katika kipindi cha takriban siku 11 mjini Kono, Miili 87 ilizikwa.

Miili ya Watu waliokufa kutokana na maradhi ya Ebola ni hatari kwa maambukizi hivyo huzikwa kwa uangalifu mkubwa ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo.