Nguo za ndani zinazowalinda wanaume

Haki miliki ya picha
Image caption Nguo hizi za ndani zinasemekana kuwa na uwezo wa kulinda wanaume kutokana na madini hatari yanayoathiri nguvu za kiume

Kampuni ya Belly Armor, ambayo ilikua ya kwanza kutengeza bidhaa zinazohitajika na wanawake wajawazito, kutokana na kitambaa maalum kinacholinda mwili kutokana na athari za madini ya chuma mwilini, imeanzisha biasharta nyingioenkwa manufaa ya wanaume.

Kampuni hii imeanza kutengeza nguo za ndani za wanaume ambao zinawalinda kutokana na athari ya madini ya chuma yanayoweza kupunguza nguvu za kiume na kuathiri uzalishaji wa mbegu za kiume hali ambayo inaweza kusababisha mwanaume kukosa kuzalisha.

Unaweza kujiuliza je biashara ya kutengeza vitambaa hivyo inanawiri? Jibu? Ndio tena sana.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Mbegu za wanaume zinaweza kuthiriwa na madini yanayotumiwa kutengeza simu za mkononi

Mnamo mwaka 2011, shirika la afya duniani lilitaja madini hayo hatari ikiwemo miale inayotokana na simu za mkononi kama yenye uwezo wa kusababisha saratani ya ubongo mbali na athari nyinginezo hatari kwa mwili kiafya.

Kwa mfano, watumjai wa Iphone, je mlijua kama mnapaswa kuzibeba simu zenu umbali wa milimita 10 kutoka kwa mwili wako kuhakikisha kuwa madini hayo hayaathiri mwili?

Licha ya kwamba utafiti mpya unahitajika kuthibitisha hili....ni wazi kwamba madini fulani yanayotumika kutengeza simu yanaweza kusababisha aina ya saratani za mwilini.

Na ndio maana kampuni ya Belly Armor ikaja na wazo la kuwatengezea wanaume nguo za ndani zinazoweza kuwakinga kutokana na athari hizo.

Pia utafiti ambao umefanywa unaonyesha kua baadhi ya miale inayotokana na vifaa kama vile simu za mkononi, Tabiti au Ipad, inaweza kusababisha mwili wa wanaume kupungukiwa na nguvu za kutengeza mbegu za kime au hata mwili kuishiwa na nguvu za kiume.