Al-Bashir asema ameishinda ICC

Rais Al-Bashir wa Sudan Haki miliki ya picha bbc

Rais Omar al-Bashir wa Sudan amedai ushindi katika mvutano wake na Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, baada ya mkuu wa mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda, kusimamisha uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu wa vitani katika jimbo la Darfur.

Rais Bashir, ambaye alishtakiwa kwa mauaji ya kikabila mwaka wa 2009, alisema ICC imeshindwa katika kile alichoeleza kuwa juhudi za ICC za kuiaibisha Sudan.

Alisema wananchi wameamua kuwa afisa yoyote wa Sudan asisallim amri kwa mahakama ya kikoloni.

Fatou Bensouda alisema Ijumaa kwamba kwa vile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halikuchukua hatua basi wanaofanya uhalifu wa vitani Darfur wamepata nguvu kuendelea na ukatili wao hasa dhidi ya wanawake na wasichana.