Raia wa Japan kuwachagua wabunge wapya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu nchini Japan Shinzo Abe wakati wa kufanya kampeni za uchaguzi wa ubunge.

Raia wa Japan wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa ubunge ulioitishwa mwezi uliopita na waziri mkuu Shinzo Abe wakati ambapo anatafuta uungwaji mkono katika mipango yake ya mabadiliko ya kiuchumi.

Abe pamoja na chama chake cha Liberal Democratic wanatarajiwa kushinda licha ya Japan kurejea tena kwenye hali mbaya ya uchumi.

Bwana Abe alichukua mamlaka mwaka 2012 ambapo aliahidi kuikwamua Japan kutoka kwa miongo miwili ya misukosuko ya kiuchumi.