Agathon Rwasa apuuza mahakama Burundi

Haki miliki ya picha none
Image caption Agathon Rwasa ni kiongozi wa kundi la zamani la waasi FNL

Hii leo mkuu wa zamani wa kundi la uasi nchini Burundi FNL Palipehutu Aghaton Rwasa hakusikilizwa na hakimu wa Burundi katika kesi inayo husu mauaji ya raia banyamulenge zaidi ya mia na 160 mwaka 2004 katika kitongoji cha gatumba nje ya mji mkuu Bujumbura.

Akiwa njiani kuelekea mahakamani kundi kubwa la wafuasi wake lilimiminika mahakamani na kukosekana njia ya kupita.

Mwanasiasa huyo amepinga kupitia risala yake kwa mwendesha mashtaka mkuu kwamba mahakama za Burundi hazina haki ya kumuhukumu kulingana na sheria rasmi kuhusu makosa ya wakati wa vita Burundi .

Mamia kadhaa ya wafuasi wa Agathon Rwasa walikusanyika na kuimba mbele ya makaazi yake mtaa wa Kiriri kwa kumuunga mkono kwamba hawezi kuchukuliwa na polisi.

Agathon Rwasa alikuwa ameelekea kwenye mahakama ya rufaa ambako pia wafuasi wake walijaa na kuzuiwa na polisi,lakini amesema hakuwa amekwenda kuitika kesi badala yake alipeleka risala inayo pinga yeye kuhukumiwa na mahakama za Burundi wakati huu.

Lori tatu na magari ya polisi zilizunguka makaazi yake Agathon Rwasa na kuwatawanya wafuasi wake walio kuwa na vibango vinavo dai kuwa hawato kubali ,Kwani ni wangapi waliuwawa wakatupwa mitoni na ziwani kwa nini sheria imuandame tu kinara wao.

Maafisaa wa polisi walojaribu kuingiz nyumbani kwake Agathon Rwasa hawakuweza kutoka na upinzani wa wafuasi hyao.Lakini hatimae Agathon Rwasa amewapa amri ya kuondoka kama hivi.

Aliwashukuru wafuasi wake kwa kumuunga mkono na kuwatakiwa kila la heri.

Agathon Rwasa ni mmoja wa wanasiasa wa upinzani alieendesha vita vya maguguni akiongoza kundi la FNL Palipehutu ambapo mwaka 2004, wakimbizi wakongomani banyamulenge walivamiwa kwenye kambi yao 166 waliuwawa na wengine zaidi ya 150 walijeruhuiwa.

Jumuia ya Banyamulenge imefungua mashitaka lakinui upande wa Agathon Rwasa wamedai hizi ni mbinu za serikali kutaka kuangusha umaarufu wake.

Baadhi ya wana siasa wa upinzani wamemuunga mkono Agathon rwaa akiwemo rais wa zamani wa mpito Domitien Ndayizeye.

Hadi sasa hakuna tarehe rasmi imetolewa kuhusu kusikilizwa tena kesi hii.