Afrika Magharibi wajadili usalama barani

Haki miliki ya picha none
Image caption Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria, kundi ambalo limetajwa kuwa katili zaidi duniani

Wakuu wa serikali kutoka nchi za Chad, Mauritania na Mali leo wanakutana katika mji mkuu wa Senegal, Dakar kwa ajili ya mkutano wa kimataifa kuhusu amani na usalama barani Afrika.

Wataalam wa masuala ya ulinzi pia nao wanahudhuria mkutano huo kujadili masuala kama vile kusambaa kwa silaha na udhibiti wa mpaka.

Haki miliki ya picha
Image caption Mmoja wa waathirika wa mashambulio ya kigaidi ya kundi la Boko Haram
Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu waliojitolea kuungana na jeshi la serikali ya Nigeria kupambana na Boko Haram

Baada ya kikao cha wakuu wa nchi zinazozungumza Kifaransa, mji mkuu wa Senegal, Dakar ni mwenyeji wa mkutano mwingine muhimu. Hii ni mara ya kwanza kwa mataifa hayo ya Afrika kuandaa mkutano wa kimataifa kuhusu amani na usalama. Wakuu wa serikali, mawaziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje, pamoja na wataalam na mashirika yasiyo ya kiserikali wanahudhuria mkutano huu. Zaidi ya wajumbe 300 watajadili masuala ya usalama barani Afrika kwa siku mbili. Lengo ni kujenga utamaduni wa usalama. Waandaaji wa mkutano huu wana matumaini kwamba utakuwa wa kawaida na tukio la kila mwaka. Kwa upande wake waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Senegal Cheikh Tidiane Gadio, amesema ni wakati ambapo mataifa ya Afrika yanatakiwa kushughulikia yenyewe masuala ya usalama barani Afrika. Migogoro mikubwa inayolikumba bara la Afrika itajadiliwa kama vile kitisho cha kundi la wapiganaji wa Kiislam wa Boko Haram.

Kundi hili kwa kiasi kikubwa linaendesha harakati zake nchini Nigeria laki wapiganaji wake wamefanya mashambulio kuvuka mipaka hadi katika nchi za Cameroon na Niger. Uchunguzi wa BBC umegundua kuwa kundi hilo limeua watu 786 katika mwezi Novemba 2014. Ushirikiano wa kikanda unaongezeka katika kukabiliana na wapiganaji hawa. Nigeria, Niger, Cameroon na Chad zimeahidi kupeleka askari 2800-watakaounda jeshi imara la kikanda na kuratibu usalama wa mpaka.