Polisi wampa kipigo mtekaji nyara Australia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Baadhi ya watu waliojeruhiwa katika uvamizi uliofanywa na raia wa Iran na kuwateka nyara watu ndani ya mgahawa

Uvamizi ambao umeendelea kwa masaa 16 nchini Australia ambapo mwanamume aliyekuwa amejihami na kuwateka nyara watu ndani ya mgahawa mmoja mjini Sydney umemalizika.

Mvamizi huyo anasemekana kuwa raia wa Iran kwa jina Haron Monis.

Katika matukio ambayo yameonyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni, polisi walifyatua risasi huku milio mikubwa ya risasi ikisikika huku baadhi ya mateka wakikimbilia usalama wao.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bwana Moni anajulikana sana na polisi kwa rekodi yake ya uhalifu

Baadhi ya watu waliojeruhiwa kufutia ufyatuaji huo wa risasi walipelekewa hospitalini. Inaarifiwa watu kadhaa wamejeruhiwa. Hali ya mvamizi huyo anayesemekana kuwa na umri wa miaka 49 bado haijajulikana.

Mwanamume huyo alikua ameachiliwa kwa dhamana kwa makosa mbali mbali aliyokuwa ameshitakiwa nayo. Moja ya makosa yake ilikuwa kuwatumia barua ya matusi wazazi wa wanajeshi wa Australia waliofariki wakiwa wanatumikia jeshi la taifa hilo nchini Iraq.

Waziri mkuu Tony Abbott alisema lilikuwa jambo la kushtua sana kwamba wananchi waiso na hatia walitekwa nyara na mtu ambaye alikuwa anashinikizwa kisiasa.

Makomando wa jeshi walifyatua risasi na kisha kuingia ndani ya mgahawa huo huku wakirusha magurunedi. Inaarifiwa watu wengi walijeruhiwa.