Wafungwa Philippines waponda raha

Image caption Wafungwa gerezani nchini Ufilipino

Polisi mjini Manila wamevamia gereza moja na kuushangaza umma wa Philippines baada ya kung'amua maisha ya anasa yanayoendelea ndani ya gereza hilo kwa kikundi cha baadhi ywa wafungwa wenye upendeleo wa kipekee.

Uvamizi huo umefanywa katika gereza hilo la Bilibid lenye wafungwa wengi nchini humo kufuatia taarifa kwamba mtandao wa dawa za kulevya nchini humo unafanya kazi katika gereza hilo kwa njia za panya.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Polisi nchini Phillipines

Baada ya uvamizi huo maafisa wa polisi walikuta wafungwa hao wakiwa wamefunga viyoyozi,mabafu ya kuogea ya kisasa yenye marumaru na kupambwa kwa mawe ya thamani,makasha ya kuhifadhia fedha,saa za gharama na fedha lukuki.

Wafungwa hao walifanikiwa pia kununua pombe kali za gharama kubwa ,komputa na hata simu za kisasa za gharama kubwa.kufuatia tukio hilo serikali ya Philippine imeahidi kufanya uchunguzi wa kina.