Idadi ya waliouawa Pakistan yafika 130

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanafunzi walionusurika

Vikosi vya usalama nchini Pakistan vinakabiliwa na hali ngumu kuweza kudhibiti shule iliyovamiwa na wapiganaji wa Taliban katika jimbo la Peshawar Kaskazini Magharibi mwa Pakistan

Takriban watu miamoja na thelathini wamefariki , wengi wao wakiwa watoto.

Msemaji wa jeshi anasema washukiwa sita wameuawa huku operesheni hio ikiendelea.

Shule hio inasimamiwa na jeshi na wanafunzi wengi ni watoto wa wanajeshi.

Wakuu wa Hospitali wanasema kuwa zaidi ya watu 40 wanasemekana kujeruhiwa japo idadi hiyo inatarajiwa kupanda zaidi.

Maafisa mjini Peshawar wanasema kuwa wanaume watano ama sita waliokuwa na silaha waliingia shuleni humo wakiwa wamevalia magwanda ya kijeshi .

Haki miliki ya picha AP
Image caption Taliban yaua wanafunzi Pakistan

Wanafunzi mia tano na waalimu walikuwa katika shule hiyo ya umma ya kijeshi wakati sham,bulizi hilo lilipotokea .

Wakazi wa eneo hilop wanasema kuwa walisikia milio ya bunduki iliyodumu kwa dakika kadhaa .

Wanasema pia kuwa walisikia sauti za kelele za wanafunzi na waalimu .

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanajeshi wakijiandaa kwa makabiliano na wapiganaji wa Taleban

Haijabainika wazi ni kwa namna gani wanamgambo wa Talebain waliweza kupenya hadi kuingia ndani ya majengo hayo yanayomilikiwa na jeshi.

Jeshi la Pakistan limesema operesheni ya uokozi ilikuwa ikiendelea na kwamba wengi wa wanafunzi na waalim wameokolewa toka eneo la hatari.

Shambulio hilo limetokea wakati operesheni kubwa ya kijeshi ikiendelea dhidi ya wapiganaji wa Taleban wa Pakistan na wanamgambo wengine wanaoendesha harakati zao kaskazini mwa jimbo la Waziristan.