Klabu bigwa-dunia Madrid yatinga fainali

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raha ya goli ni shamra shamra, wanapongezana

Wakicheza katika dimba la Stade de Marrakech. Mjini Marrakech Nchini Morocco, Mabingwa wa Ulaya Real Madrid wamepata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Cruz Azul na kutinga Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.

Real Madrid walianza kupata magoli yake dakika ya kumi na 15 kupitia kwa beki Sergio Ramos mshambuliaji Karim Benzema akaongeza la pili dakika ya 36,

Kipindi cha Pili, Gareth Bale, alifunga bao la 3 na Isco, kuhitimisha kwa goli la 4 na kuipelea Madrid fainali.

Azul walikosa penati dakika ya 40 iliyopigwa na Gerardo Torrado, na kuokolewa na kipa Iker Casillas.

Real wanasubiri mshindi wa mchezo wa leo kati ya San Lorenzo ya Argentina na Auckland City ya New Zealand.