Paul Walsh:hawanii uwenyekiti Formula1

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Madereva wa Formula one wakiwa kazini.

Boss wa zaman wa Diageo Paul Walsh amejiondoa mwenyewe kwenye kinyanganyiro cha kuwania uwenyekiti wa Formula1.

Ilikua ikidhaniwa kuwa Walsh alikua na mpango binafsi wa kuwa mbadala wa mwenyekiti wa sasa Peter Brabeck-Letmathe.

Paul Walsh, mwenye umri mwa miaka 84 alikutana na mwanasheria wa Fomula1 Sacha Woodward-Hill, kumueleeza kujitoa kwake japokuwa alionekana ni mtu sahihi kutwaa nafasi hiyo ya uongozi.

Habari za Walsh zimekuja huku kukiwa na uchunguzi wa kuchunguza tuhuma za kuwakimbia Ecclestone baada ya mgogoro wa kifedha baina ya timu mbili za Marussia na Caterham.

Mwenyekiti wa hivi sasa Peter Brabeck-Letmathe anasumbuliwa na maradhi na huenda akajiuzulu.