Kijana mzungu abadilika kuwa m'masai

Haki miliki ya picha J SANCHEZ
Image caption KIjana mmoja raia wa Sweden amegeuka na kuwa kijana wa kimasai

a kimasai nchini kenya.Aliposafiri nchini Kenya mwaka 2011 kama mtu aliyejitolea katika shirika moja lisilo la kiserikali ,uamuzi wa kuwa kijana wa kimasai wa Ilchamus lilikuwa wazo la mwisho katika akili ya Max Roing,ambaye ni raia wa Sweden.

Lakini miaka mitatu baadaye ,Max mwenye umri wa miaka 25 amependa sana utamaduni wa watu hao walio wachache katika fukwe za ziwa Baringo.

Max pia alikuwa miongoni mwa vijana 5,000 wa Ilchamus katika kaunti ya Baringo waliotawazwa kuwa wanaume kamili baada ya kupashwa tohara.

Image caption Vijana wa kimasai wakihitimishwa kuwa wanaume kamili baada ya kupashwa tohara

''Nilikuja nchini Kenya kama mtalii na pia kusaidia kuhifadhi mazingira kupitia upandaji wa miti katika kaunti ya kajiado''bwana Roing aliliambia gazeti la Nation nchini Kenya baada ya kuhitimu.

Kwa sasa anafuata mila yake mpya inayoshirikisha mavazi yanayovaliwa pamoja na shuka nyeusi,simi iliofungwa katika ukanda wake wa rangi ya hudhurungi,viatu vyeusi na nguo iliorembeshwa kwa shanga.

Hafla hiyo ya kuhitimu imemfanya kuingia katika umri wa Ilmeng'ati.

''Mimi ni Max Lemeyan Le Kachuma kutoka kabila la Ilchamus na ukoo unaojiita Iltoimai''alisema jina lake huku akinywa maziwa yalio chungu katika kikombe.