Marekani na Cuba kuimarisha uhusiano wao

Image caption Rais wa Marekani Barrack Obama na mwenzake wa Cuba Raul Castro wanasalimiana.wawili hao wametangza kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia ambao umezorota katika kipindi cha miaka 50 iliopita.

Marekani na Cuba zinatarajiwa kuanza mazungumzo ili kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia katika hatua ya kihistoria kati ya mataifa hayo mawili.

Marekani pia ina mpango wa kufungua ubalozi mjini Havana mwezi ujao.

Hatua hiyo ni mpango wa makubaliano uliosababisha kuachiliwa kwa Allan Gross na Cuba na unashirikisha kuachiliwa huru kwa raia watatu wa Cuba waliofungwa jela mjini Florida kwa upelelezi.

Rais wa Marekani Barrack Obama baadaye atasherehekea umuhimu wa mabadiliko ya sera za Marekani kuhusu Cuba katika kipindi cha miaka 50.

Obama na rais wa Cuba Raul Castro wote wanatarajiwa kutoa tangazo la mpango huo.

Bwana Gross aliwasili katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Andrews Airforce Base karibu na mjini Washington kutoka Cuba siku ya jumatano.

Kanda za video zimemuonyesha akitoka katika ndege ya serikali ya Marekani ambapo alilakiwa na kundi moja la watu.