Tetesi za usajili Barani ulaya

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption David De Gea

Real Madrid wako tayari kuvunja rekodi ya usajili kwa kumsajili mlinda mlango David De Gea toka klabu ya Man United usajili huu utavunja rekodi ya uhamisho iliyowekwa na kipa Gianluigi Buffon aliehamia Juventus toka Parma.Huku kukiwa na taarifa De Gea anafuraha kubaki na kikosi cha Manchester United na atasaini mkataba mpya .

Timu ya Liverpool imefikia makubaliano ya kumsajili kipa Guillermo Ochoa toka klabu ya Malaga kwa dau la £3milion ili kuwa mbadala wa Simon Mignolet ambae ameporomoka kiwango msimu huu.

Crystal Palace wanafanya mpango kumsajili kwa mkopo beki Ashley Cole mwenye miaka 33 toka klabu ya As Roma ya Itali.

Manchester United na Manchester City wako tayari kutoa dau la £20milion ili kuweza kumtwaa kiungo Ivan Rakitic wa klabu ya Barcelona.

Bosi wa Real Sociedad David Moyes anaimani ya kumpata kwa mkopo mshambuliaji Adnan Januzaj mwenye miaka 19, Januzaj alingara sana enzi za utawala wa kocha Moyes akiwa na Man United.

Meneja wa Sunderland Gus Poyet anataka kuongeza makali ya safu yake ya ushambulaji kwa kumsajili mshambuliaji Danny Ings toka klabu Burnley.

Tottenham wako tayari kuwaachia washambuliaji wake Emmanuel Adebayor na Roberto Soldado ili kupata pesa itakayotumika kumsajili mshambuliaji wa Fc Porto Jackson Martinez.