Vaan atwaa tuzo ya kocha bora- holland

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Van Gaal

Louis van Gaal ameteuliwa kuwa kocha bora wa mwaka wa Uholanzi baada ya kuliongoza taifa hilo kufika nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia nchi Brazil.

Kocha huyo aliacha kazi ya kuinoa timu ya taifa baada ya kupata dili la kuwa kocha wa klabu ya Manchester United alikabidhiwa tuzo hiyo jana katika jiji Amsterdam nchi Uholanzi.

Winga machachari wa timu ya taifa na klabu ya Bayern Munich Arjen Robben ameibuka kuwa mwanamichezo bora wa mwaka wa Uholanzi.

Huku mshambuliaji Robin van Persie akitwaa tuzo ya goli bora kwa goli la kichwa alilofunga kwenye michuano ya kombe la dunia dhidi yan Hispania.

Dereva wa kinda wa fomula1 Max Verstappen,ameibuka kidedea katika tuzo za mwanamichezo bora chipukizi, skater Ireen amekua mwanamichezo bora wa kike baada ya kufanya vizuri kwenye michezo ya Olimpiki.