Spika Zziwa ang'olewa Afrika Mashariki

Image caption Dk.Margaret Nantongo Zziwa,aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki,EALA

Bunge la Afrika Mashariki limemwondoa madarakani spika wake Margaret Nantongo Zziwa kutokana tuhuma mbalimbali.

Kuondolewa kwa Dk. Zziwa kulipitishwa na theluthi mbili ya wabunge waliochaguliwa wa bunge hilo.

Kwa sasa bunge hilo litaendelea na uchaguzi wa kumpata spika mpya kutoka Uganda, ambako anatoka Spika Zziwa aliyeng'olewa madarakani, lakini kwa mujibu wa sheria za bunge hilo ambazo nafasi hiyo ni ya mzunguko, Spika mpya wa bunge hilo atalazimika kuwa mbunge kutoka Uganda.

Wabunge wa EALA kwa muda mrefu wamekuwa katika harakati za kumtoa Bi Zziwa kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ya ofisi.

"hatimaye tumefanikiwa kupata kile tulichokuwa tukitaka na tunatarajia tutamchagua spika mpya ambaye atatuongoza kwa mwaka mzima mwaka ujao tutakaporejea kuendelea na vikao vya bunge," amesema mbunge wa EALA kutoka Kenya Peter Mathuki.

Dk. Zziwa alisimamishwa wadhifa wake wa Spika kufuatia hoja iliyopitishwa na wabunge wa EALA mwezi Novemba katika kikao chake cha mjini Nairobi akizuiwa kutekeleza majukumu yake ya Spika wakati huo akisubiri uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Mbunge wa Uganda Chris Opoka-Okumu anakaimu nafasi hiyo kutekeleza majukumu yanayohusiana na kumng'oa Spika