Naibu spika amwagiwa maji bungeni Kenya

Image caption Naibu spka Joyce Laboso ambaye amemwagiwa soda

Kikao cha adhuhuri cha wabunge nchini Kenya, kinaendelea kuzua hisia kali huku wabunge wakiendelea kuvurugana humo.

Wabunge hao wanajadili mswada tatanishi wa usalama ambao upande wa upinzani unasema unakwenda kinyume na katiba na kuwanyima wakenya haki yao ya kujieleza.

Mmoja wa wabunge hao wa upinzani amemwagia soda naibu spika Joyce Laboso ambaye alikuwa anasimamia kikao hicho cha kufanyia mswada huo mabadiliko kabla ya kupitishwa.

Spika wa bunge hilo sasa amechukua usukani na kuamuru kutimuliwa kwa wabunge wawili waliokuwa wamezidi vurugu.