Wanajeshi wahukumiwa kifo Nigeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanajeshi nchini Nigeria

Mahakama ya Nigeria imewahukumu kifo wanajeshi 54 waliobainika na makosa ya uhaini.

Wanajeshi hao wanadaiwa kuwa walikataa kwenda katika miji iliyopo kaskazini mwa nchi hiyo kukabiliana na wapiganaji wa kundi la Boko Haram. Hata hivyo washitakiwa hao wamekana mashitaka hayo.Wanasheria wa washitakiwa hao wamesema kuwa watano kati yao walikuwa hawana hatia katika kesi iliyoendeshwa ndani ya mahakama.

Makundi ya kijeshi yanayopigana na Boko Haram kaskazini mwa Nigeria wamekuwa wakilalamikia uhaba wa vifaa hali ambayo inasababisha wengine kutoroka.