Watu 33 wauawa,100 watekwa Nigeria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapiganaji wa kundi la Boko Haram

Wanamgambo wamevamia kijiji kimoja kazkazini mashariki mwa Nigeria na kuwaua takriban watu 33 na kuwateka wengine 100,mmoja ya waathiriwa amesema.

Amesema kuwa washukiwa wa kundi la Boko haram waliwakamata vijana wadogo,wanawake na watoto kutoka kijiji cha Gumsuri.

Shambulizi hilo lilitokea siku ya jumapili lakini habari hizo zilibainika baada ya waathiriwa kufika mji wa Maiduguri.

Wakati huohuo,jeshi la Cameroon limesema kuwa limewaua wanamgambo 116 ambao walikuwa wameshambulia kambi moja ya kijeshi kulingana na AFP.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Moja ya vijiji vilivyoavamiwa na wanamgambo wanaodaiwa kutoka kwa kundi la Boko haram

Wakaazi wameiambia BBC kwamba wanamgambo waliojihami na silaha walishambulia eneo la mpakani la Amchide siku ya jumatano,walipowasili kwa magari mawili huku wengine wakitembea.

Walivamia eneo la soko na kuchoma maduka na zaidi ya nyumba 50.

Hakuna kundi lililokiri kutekeleza mashambulizi hayo lakini maafisa wamelaumu wapiganaji wa Boko Haram.

Zaidi ya watu 2000 wameuawa katika ghasia za makundi yaliojihami na silaha mwaka huu pekee,hususan kazkazini mwa Nigeria karibu na mpaka na Cameroon.