Kikwete aahirisha hotuba yake.

Image caption Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete

Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameahirisha kulihutubia taifa la nchi hiyo kama ilivyokuwa imetarajiwa .

Kwa muujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais badala yake Rais Kikwete atalihutubia taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar Es Salaam, mchana wa Jumatatu, Desemba 22, 2014.

Taarifa hiyo fupi inasema wakati wa mazungumzo yake na Wazee hao, Rais Kikwete atazungumzia masuala mbali mbali ya kitaifa, yakiwemo yale ambayo yamekuwa yanasubiri maamuzi yake tokea alipokuwa anajiuguza kufuatia upasuaji aliofanyiwa mwezi uliopita .