Korea kazkazini sasa yaionya Marekani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais wa Korea Kazkazini Kim Jong un .

Korea Kazkazini sasa inataka uchunguzi wa pamoja na Marekani kufanywa kuhusu wizi wa mtandaoni uliosababisha kampuni ya Sony Pictures kuahirisha maonyesho ya filamu ya ucheshi inayomdhihaki raia wa Korea kazkazini Kim Jong-un.

Imesema kuwa shtuma hizo za shirika la ujasusi nchini marekani FBI kwamba Pyongyang ndio iliotekeleza uovu huo inaliharibia jina taiafa hilo.

Chombo rasmi cha habari nchini humo kilimnukuu waziri wa maswala ya kigeni ambaye jina lake halikutajwa akisema kuwa taifa lake litachukua hatua kali iwapo Marekani itakataa ombi hilo.

Taifa la Korea Kazkazini hapo awali lilikuwa limeunga mkono uvamizi huo wa kampuni ya Sony likisema kuwa ni kitendo cha haki.

Rais Obama amesema kuwa Marekani itajibu shambulizi hilo la mtandaoni wakati utakapowadia.