Marekani yaitupia lawama Korea kaskazini

Haki miliki ya picha fdd
Image caption Katikati ni kiongozi wa Korea kaskazini Kim jong_un

Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.

Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala wake utafanya hivyo baada ya kuilaumu nchi hiyo kufanya uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures.

Amesema mara tu mchakato wao huo utakapokamilika, watajibu mashambulizi hayo. Korea kaskazini imeziita tuhuma hizo zilizotolewa na Marekani dhidi yake kuwa ni za uzushi.

Korea kaskazini ilikuwa katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, kabla ya kuondolewa wakati wa utawala wa Rais George Bush wa Marekani mwaka 2008.