Niger kuwakabili Nigeria kombe la Afrika

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kikombe cha CAF

Shirikisho la soka barani Afrika Caf limetangaza ratiba ya michuano ya kombe la Afrika kwa vijana, itakayofanyika nchini Niger 2015.

Wenyeji wa michezo hiyo Niger walio kundi A wataanza kuwakabili Nigeria huku mchezo mwingine wa kundi A utawakutanisha Guinee na Zambia.

Michezo ya kundi B Ivory Coast wataanza kwa kumenyana na Afrika kusini kundi huku Mali wakiwakabili Cameroon

Fainali za michuano hiyo ya vijana chini ya umri wa miaka 17, itafanyika kuanzia February 15 mwaka 2015 huko nchi Niger.

Ligi kuu Tanzania kupigwa mwisho wa wiki

Baada ya kusimama kwa takribani miezi miwili ligi kuu nchi Tanzania. inatarajiwa kuanza tena kutimua vumbi mwishoni mwa wiki.

Timu nyingi zikiwa zimeimarisha vikosi vyao kabla ya kuanza kwa duru ya pili kwa kusajili wachezaji wapya, Vigogo Simba imewasajili washambuliaji ndugu Dan Serunkuma,na simon serunkuma na beki juuko murishid toka Uganda.

Mabigwa watetezi Azam wamejimarisha kwa kuwasajili Amri kiemba,Paschal Wawa toka El merreik ya Sudan na Bryan Majwega toka uganda.

Huku Yanga wakibadilisha bechi lao la ufundi kwa kumtimua Mbrazil Marcio Maximo na msaidizi wake Leonardo Leiva na kumteua Hans Pluijm kuwa kocha mkuu wa timu hiyo akisaidiwa na Charles Boniface mkwasa.

Mtibwa Sukari ya morogoro ndio vinara wa ligi wakiongoza kwa pointi 15 baada ya kushuka dimbani mara 7 wakifuatiwa na yanga wenye pointi 13.Timu ya Mbeya City ndio wanaburuza mkia wakiwa na pointi 5.