USA yaitaka K.Kazkazini kuilipa Sony

Haki miliki ya picha
Image caption Wakuu wa kampuni ya filamu ya Sony Pictures.Marekani imeitaka Korea Kazkazini kuilipa kampuni hiyo kwa hasara iliopata baada ya madai ya kuhusika na uhalifu wa mtandao dhidi yake

Marekani imezitaka China na nchi zingine kuthibitisha kuwa Korea Kaskazini ilihusika na uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures.

Marekani inasema kuwa Korea Kaskazini ni lazima ikiri kuwa ilihusika na iilipe Kampuni ya Sony kutokana na hasara ambayo imepata

Korea Kaskazini imeyataja madai hayo ya Marekani kuwa ya uongo.

Wataalamu wanasema kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa Korea Kaskazini ilihusika.

Lakini mwandishi wa BBC nchini Korea Kusini anasema kuwa kampuni ya Sony Pictures nchini Marekani na wakuu wake nchini Japan watahitajika kuamua iwapo wataonyesha filamu ya uchesi yenye utata ya rais wa Korea Kazkazini Kim Jong-un.