Tunisia kumchagua mrithi wa Ben Ali.

Raia wa tunisia wapiga kura ya kumchagua rais mpya wa taifa hilo tangu kuondolewa kwa Abedinne Ben Ali

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Raia wa tunisia wapiga kura ya kumchagua rais mpya wa taifa hilo tangu kuondolewa kwa Abedinne Ben Ali

Raia wa Tunisia wanapiga kura hii leo katika raundi ya pili na ya mwisho ya kile kinachoonekana kama uchaguzi wa rais wa kihistoria.

Ni uchaguzi unaotarajiwa kuleta demokrasia nchini humo,ambao unajiri miaka minne tangu kuondolewa madarakani kwa Zine Abedine Ben Ali.

Wagombea wa sasa ni kaimu rais Moncef Marzouki ambaye amekuwa mwanaharakati wa haki za kibinaadamu kwa muda mrefu na Beiji Caid Essebsi mwenye umri wa miaka 80 ambaye amehudumu katika serikali zilizopita.

Alishinda kura nyingi wakati wa raundi ya kwanza .

Usalama umeimarishwa nchini humo baada ya wapiganaji wa Jihad kutishia kuchafua uchaguzi huo.