Kura zaanza kuhesabiwa Liberia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kura zaanza kuhesabiwa nchini Liberia baada ya uchaguzi wa usineta kufanyika

Kura zimeanza kuhesabiwa nchini Liberia ambapo uchaguzi wa Useneta umefanyika licha ya mlipuko wa ebola.

Idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilikuwa chini huku watu wengi wakisalia majumbani mwao kwa hofu ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Viwango vya joto vya wapiga kura vilichukuliwa ,huku wakiambiwa kusimama kwa umbali wa mita moja mmoja baada ya mwengine na kuosha mikono yao kabla ya kupiga kura na hata baada ya kushiriki katika shughuli hiyo.

Matokeo ya mapema yanatarajiwa baadaye siku ya jumapili.

katika mji mkuu wa Monrovia ,mwana wa rais Ellen Johnson Sirleaf anakabiliana na mwanasoka mkongwe George Weah ambaye aliwania urais mwaka 2005.