Michael Carrick ni mchezaji bora

Haki miliki ya picha PA
Image caption Michael Carrick

Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema Michael Carrick ndie mchezaji bora wa kingereza kwa sasa.

"Nadhani Michael ndie kiungo bora wa kati katika kandanda ya Uingereza," amekua katika kiwango bora Zaidi kwa sasa” alieleza Ferguson.

Ferguson alimsajili Carrick,ili kuja kuwa mbadala wa kiungo Roy Keane, mwaka 2006. Tangu amekua mmoja kati ya viungo bora kwa Man United na timu yataifa ya England.

Carrick ameteuliwa kuwa nahodha msaidizi wa Man United, baada ya kurudi uwanja kutoka kwenye maumivu ya kifundo cha mguu.

Kiungo huyu alijiunga na Mashetani wekundu mwaka 2006 akitokea klabu ya Tottenham amekua msaada mkubwa kwenye safu ya kiungo na msimu huu amekua akitumika kama mlinzi kwa kucheza namba 5.