Sony yamfurahisha Rais Obama

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kampuni ya Sony

Rais wa Marekani amelipokea kwa furaha tangazo la kampuni ya Sony kuamua kuonyesha filamu ya kuchekesha yenye utata 'The Interview

Filamu hiyo itaoneshwa katika baadhi tu ya kumbi za sinema nchini Marekani mnamo siku ya Krismas.

Rais Obama awali aliikosoa kampuni hiyo kwa kusitisha mpango wake wa uzinduzi wa filamu hiyo inayohusu kuuawa kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, baada ya shambulizi la mtandao dhidi ya kampuni ya Sony linaloaminika kufanywa na Korea Kaskazini.

Baadhi ya watu waliokuwa wakisubiri kununua tiketi katika jimbo la Virginia wameelezea kwa nini wanataka kuiona sinema hiyo;

Nadhani ina hamasa fulani, na nadhani itafurahisha kuona nini kitatokea baadae, kisiasa na katika ulimwengu wa sasa ambapo jamii na kila mmoja anaishi. Nitapenda kuitizama hiyo sinema. Nadhani itakuwa ni vizuri sana kuangalia sinema inayochekesha lakini pia ina ukweli ndani yake. anasema Spencer James.