Kijana mwingine mweusi auawa Marekani

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Eneo la tukio St Louis

maandamano makubwa yametokea nchini Marekani katika mji wa St Louis yaliyosababishwa na askari kumpiga risasi kijana mweusi akiwa katika kituo cha mafuta .Polisi wanamtetea afisa mwenzao ya kwamba alitenda kitendo hicho kama njia ya kujihami ,baada ya marehemu kumnyoonyeshea bunduki katika kitongoji cha Berkeley.

Waandamanaji waliyaanza maandamano hayo mara tu baada ya taarifa za mauaji hayo kusambaa,kutokana na hasira waliyonayo waandamanaji hao picha za video zinawaonesha baadhi yao wakivuka mpaka waliowekewa na polisi .

kitongoji cha Berkeley kiko umbali wa kilomita tatu kutoka mjini Ferguson, Missouri, mahali ambako yalifanyika mauaji ya kijana mwingine mweusi aliyekuwa na umri wa miaka kumi na nane Michael Brown , aliyepigwa risasi na askari wa kizungu,mauaji yaliyoibua hisia za ubaguzi wa rangi ,mauaji ambayo yalitokea mwezi August mwaka huu .hata hivyo Brown hakuwa na silaha yoyote wakati akiauwa.