Wanawake madereva Saudia mashakani

Haki miliki ya picha AP
Image caption Wanawake madereva waingia mashakani saudia

Wanawake wawili wa Saudi Arabia waliokamatwa kwa takriban mwezi mmoja kwa kukiuka marufuku ya wanawake kuendesha magari nchini humo wamepelekwa katika mahakama inayosikiliza kesi za ugaidi.

Mawakili wa wanawake hao wamekataa rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Mmoja wao Loujain Hathloul alikamatwa baada ya kujaribu kuendesha gari kuingia katika ufalme huo kutoka umoja wa milki za kiarabu.

Maysaa Alamoudi mwandishi kutoka milki za kiarabu aliwasili katika mpaka huo kumsaidia Hathloul na ndiposa akakamatwa.

Baadhi ya watu wa karibu wa wanawake hao wawili wanasema kuwa wanashtakiwa sio tu kwa kukiuka marufuku hiyo bali kwa maoni yao walioweka katika mitandao.