Song atemwa katika kikosi cha Cameroon

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kikosi cha Cameroon.Kiungo wa kati wa timu hiyo ametemwa katika kikosi

Kocha wa Cameroon Volke Finke ametaja kikosi cha Cameroon chenye wachezaji 24 kitakachoshiriki katika mechi za kombe la Afrika nchini Equitorial Guinea.

Kocha huyo amekitaja kikosi kilekile cha wachezaji walioshiriki katika mechi za kufuzu,laki akamuwacha nje kiungo wa kati wa timu ya West Ham Alexander Song.

Mchezaji huyo hajaichezea Cameroon tangu apewe kadi nyekundu wakati timu hiyo ilipofungwa mabao 4-0 na Croatia wakati wa kombe la dunia.

Kuimarika kwa mchezo wake katika kilabu ya West Ham msimu huu,kulizua uvumi kwamba huenda akashirikishwa katika kikosi hicho.