Uturuki: Kijana akamatwa kumtukana Rais

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki

Polisi nchini Uturuki wamemkamata mwanafunzi wa sekondari mwenye umri wa miaka kumi na sita kwa tuhuma za kumtukana Rais Recep Tayyip Erdogan.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, kijana huyo alipelekwa mahabusu baada ya kumtuhumu Bwana Erdogan na chama chake tawala cha AK kwa vitendo vya rushwa wakati wa mkutano wa hadhara katikati ya mji wa Anatolia.

Waziri Mkuu Ahmet Davutoglu ametetea kukamatwa kwa mwanafunzi huyo akisema ofisi ya rais lazima iheshimiwe.

Kumtukana mkuu wa nchi ni makosa kwa mujibu wa sheria za Uturuki na mwanafunzi huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka minne jela endapo atapatikana na kosa.