Korea Kazkazini yamtusi Obama

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Barrack Obama wa marekani amefananishwa na tumbili wa msitu wa Tropiki

Korea kaskazini imeilaumu Marekani kutokana na mataizo ya mtandao ambayo yameikumba siku chache zilizopita.

Tume ya taifa ya ulinzi nchini Korea Kaskazini inasema kuwa Marekani inavuruga mifumo ya mitandao ya nchi hiyo huku ikimfananishi rais wa marekani Barack obama na tumbili wa misitu ya tropiki mbali na kumshutumu kwa kuhusika katika kuonyeshwa ka filamu yenye utata inayojulikana kama The Interview.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Filamu ya the interview ambayo rasi Obama alishinikizwa ionyeshwe

Filamu hiyo iliyotengenezwa na kampuni ya Sony ambayo ni ya ucheshi inayoonyesha kuuawa kwa kiongozi wa korea kaskazini Kim Jong Un.

Korea kaskazini imekana kuhusika kwenye uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony uliosababisha kampuni hiyo kusitisha maonyesho ya filamu hiyo.