Watoto wazuiwa kuitembelea Israel

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watoto waliotekwa Gaza ndani ya Basi

Kundi la Hamas limewazuia kundi la watoto kutoka ukanda wa Gaza wengi wakiwa ni wale waliowapoteza wazazi kwenye vita vya hivi majuzi kati ya Hamas na Israel waliotaka kuitembelea Israeli katika ziara ambayo waandalizi wake wanasema ililenga kuleta uwiano. Msemaji wa Hamas anasema kuwa ziara hiyo ilizuiwa ili kulinda tamaduni ya watu wa ukanda wa Gaza.

Wapiganaji wa kundi la Hamas wamezuia kundi la watoto kutoka Gaza wengi wao wakiwa ni wale ambao wazazi wao waliuawa katika vita.

Wanaharakati wa masuala ya Amani waliowasaidia watoto hao kufanya safari hiyo wamesema kuwa mamlaka ya Gaza waliruhusu watoto hao kufanya safari yao lakini wakabadili msimamo wao baadae.