Hatukushambulia raia Somalia:Marekani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mpiganaji wa Al Shabab

Marekani imesema kuwa bado inatafakari matokeo ya shambulio la anga lililofanyika Kusini mwa Somali kumlenga kiongozi mwandamizi wa kundi la wapiganaji wa Al Shabab.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ndege za Marekani

Msemaji wa idara ya usalama ya Marekani amesema shambulio la anga katika karibu na eneo la Saakow halikuwa na dalili zozote za kuleta madhara kwa raia na hakuna raia waliodhurika.

Shambulio hilo limetekelezwa siku chache tangu mtu anayedhaniwa kuwa ni mfuasi wa kundi hilo kushambulia kambi ya majeshi ya Somalia na Jeshi la Muungano wa Afrika.