Ndege iliyopotea: Utafutaji waendelea

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Ndugu wa abaria waliopotea kwenye ndege ya AirAsia wakilia kwa uchungu

Zoezi la anga na majini la utafutaji wa ndege ya AirAsia aliyoanguka ikiwa na watu 162 baada ya kuwepo kwa dhoruba katika pwani ya eneo la Borneo siku ya jumapili imeendelea.

Maafisa wa Indonesia wanasema japo zoezi hilo limeendelea lakini linakabiliwa na upinzani kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kufuatia kupatikana kwa vipande vya mabaki ya ndege hiyo siku ya jumannne, kiongozi wa taasisi ya uokoaji na utafutaji amesema miili mitatu imepatikana hadi sasa kutoka katika eneo la bahari ya Java.

Wapiga mbizi wa kikosi cha maji cha jeshi wanatarajiwa kuanza kutafuta miili na kinasa sauti cha ndege hiyo katika kina cha chini cha maji katika eneo linalosadikiwa ndipo ndege hiyo ilipoangukia.

Ndege hiyo ilipotea ikiwa safarini ikitokea mji wa Surabaya nchini Indonesia kuelekea nchini Singapore.