Rais wa Kenya amteua mkuu mpya wa Polisi

Image caption Joseph Chirchir Boinet ameteuliwa kama inspekta jenerali mpya wa polisi nchini Kenya

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemteua Joseph Chirchir Boinet kuwa inspekta jenerali mpya wa polisi.

Boinet anachukua mahala pake David Kimaiyo ambaye alistaafu kutokana na mauaji ya wafanyikazi 36 waliokuwa wakifanya kazi katika timbo moja huko Mandera kazkazini mashariki mwa Kenya.

Boinet amekuwa katika idara ya upelelezi tangu mwaka 1998.