Mtoto albino atekwa nyara Tanzania

Image caption Albino Tanzania

Polisi nchini Tanzania wanasema kuwa wamewakamata watu saba kutokana na kutekwa nyara kwa msichana mmoja albino.

Msichana huyo wa miaka 4, Pendo Emmanuelle Nundi alitekwa siku ya jumamosi kutoka nyumbani kwao katikamkoa wa Mwanza kaskazini.

Msemaji wa Polisi Valentino Mlowola amesema kuwa baba yake mtoto huyo ni miongoni mwa wanaochunguzwa ,ili kujaribu kujua iwapo bado yuko hai.

Utafiti wa Umoja wa Mataifa unasema kuwa takriban albino 74 wameuawa nchini Tanzania ambapo vipande vya miili yao huuzwa kama vivutio vya bahati kwa takriban dola mia sita.