Mwaka Mpya: Maafa China 35 wafariki

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Umatti wa watu waliokanyagana na wengine kufa nchini China wakati wakiupokea mwaka mpya 2015

Sherehe za kuupokea mwaka mpya 2015 zimeguka kuwa majonzi baada ya watu thelathini na watano kufa kwenye taharuki ya kukanyagana kwenye msongamano wakati wakiiupokea mwaka mpya.

Maafa hayo yametokea katika mji Shanghai ambapo maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika ili kuupokea mwaka mpya.

Chanzo cha taharuki hiyo bado haijafamika lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimenukuliwa vikisema imetokana na maelfu ya watu kuzuiwa kugombea fedha bandia zilizotupwa eneo hilo kutoka katika jengo moja.