Kesi ya Greste na wenzake kurudiwa Misri

Image caption Mwandishi Peter Greste wa Aljazeera na wenzake wawili waliokamatwa nchini MIsri.Kesi ya watatu hao inatarajiwa kuanza upya.

Mahakama ya juu nchini Misri imeamuru kurudiwa kwa kesi ya waandishi watatu wa Al- Jazeera waliohukumiwa kwa madai ya kuhusika na kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.

Watatu hao hata hivyo watasalia jela hadi kesi yao itakaposikizwa tena.

Hakuna tarehe ambayo imetengwa rasmi lakini mawakili wao wanasema kuwa kesi yao itatajwa katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.

Watatu hao ni pamoja na raia wa Australia Peter Greste, raia wa Misri na Canada Mohamed Fahmy na mwengine wa Misri Baher Mohamed.

Walikamatwa mwezi Decemba mwaka 2013.