Van Gaal amlenga beki wa Aston Villa

Image caption Beki wa Kilabu ya Aston Villa Ron Vlaar alengwa na manchester united

Mchezaji Ron Vlaar analengwa na mkufunzi Louis Van Gaal huku kocha huyo akitafuta njia za kuimarisha safu yake ya Ulinzi ,ijapokuwa hakuna mawasiliano yoyote kati ya Aston Villa na Manchester United kuhusu mchezaji huyo.

Ujuzi wa Vlaar umemfanya kulengwa na Van Gaal huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akihudumu kwa msimu wake wa tatu katika kilabu ya Villa.

Vlaar alikuwa mmoja ya wachezaji waliosimamiwa na Van Gaal nchini Brazil na huku nahodha huyo akidaiwa kumaliza kandarasi yake katika kilabu ya Villa mwishoni mwa msimu huu ,huenda akawa bei rahisi iwapo meneja Van Gaal atamhitaji katika dirisha la uhamisho linaloanza siku ya jumamosi.