Waliohusika na mapinduzi Gambia wasakwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Gambia yahya Jammeh aliyeepuka jaribio la mapinduzi.baadhi ya watu waliohusika na mapinduzi hao wameanza kukamatwa

Watu kadhaa wamekamatwa na kuzuiliwa, kufuatia jaribio la mapinduzi ya hapo Jumanne dhidi ya kiongozi wa nchi hiyo, Yahya Jammeh.

Waliokamatwa ni pamoja na maafisa kadhaa wa kijeshi pamoja na raia.

Wanajeshi watiifu kwa rais, wanasemekana wamekuwa wakisaka nyumba za wapinzani wake.

Awali akiwa katika mji mkuu Banjul, Rais Jammeh alilaani washukiwa hao wa mapinduzi wanaosemekana kuungwa mkono na baadhi ya mataifa ya kigeni.