Harakati za kuokoa meli zaendelea Italia

Haki miliki ya picha epa
Image caption Wahamiaji wakisafiri katika meli ya mizigo

Askari wanaolinda pwani ya Italia wanajaribu kuwasaidia watu waliokwama ndani ya meli moja ya kibiashara, iliyotelekezwa katika pwani ya kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Meli hiyo ina zaidi ya wahamiaji haramu wapatao mia nne. Hakuna mhudumu yeyote au nahodha kwenye meli hiyo.

Hali mbaya ya hewa inaripotiwa kukwamisha shughuli za uokoaji, ambapo watu hao wanajaribu kuhamishiwa ndani ya meli ya Sierra Leone, inayobeba mifugo.