Wavulana 40 watekwa na Boko Haram

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakr Shekau.kundi hilo limedaiwa kuwateka vijana 40 katika kijiji cha Malari kazkazini mwa Nigeria

Takriban wavulana 40 na vijana wadogo wameripotiwa kutekwa nyara na wapiganaji wa kundi la Boko haram Kazkazini mashariki mwa Nigeria.

Wakaazi waliokitoroka kijiji cha Malari na kuwasili katika mji wa Maiduguri siku ya ijumaa usiku wanasema kuwa kitendo hicho kilitekelezwa siku moja tu kabla ya mwaka mpya.

Wanasema kuwa watu waliojihami waliwasili katika kijiji hicho katika gari aina ya pick up na kuwaagiza wanaume wote kutoka nje ili kuweza kusikiliza mahubiri.

Vijana wadogo baadaye walizungukwa na kupelekwa katika msitu jirani wa Sambisa.

Mwaka uliopita kundi hilo la Boko haram liliwateka nyara zaidi ya wasichana 200 kutoka shule moja ya bweni kazkazini mwa Nigeria.