Walaani msako wa wanamapinduzi Gambia

Haki miliki ya picha
Image caption Wanaharakati wa haki za kibinaadamu walaani kukamatwa wa waliohusika na mapinduzi Gambia

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamelaani hatua ya kuwakamata watu inayoendelea nchini Gambia baada ya jaribio la mapinduzi siku ya Jumanne.

Makundi hayo yanayoshirikisha kundi la Amnesty International, kundi la kutetea haki za binadamu nchini Senegal la RADDHO yalitoa taarifa ya pamoja ya kulaani kile yalichokitaja kuwa kukamatwa kwa watu kwa nia ya kuzua hofu.

Rais Yahya Jammeh ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 20 alirejea nchini humo siku ya Jumatano na kuapa kuwatafuta wale waliohusika katika jaribio la kutaka kuipindua serikali yake.